Kwako wewe usiyeamini

USHUHUDA…
BWANA Yesu asifiwe, leo ninao ushuhuda kwako, wewe usiyeamini ya kuwa Yesu wa Nazareth na Neno la Mungu ni hai hata sasa!
JUMANNE YA WIKI HII(14/08/2012), Yesu wa Nazareth amemponya kijana mmoja Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo sugu (Chronic Ulcers) ambao amekuwa nao kwa zaidi ya Miaka 7.
Kijana huyu nimekutana naye kwenye Ibada zinazoendelea kila jioni pale Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)

kwa ajili ya Wanafunzi wa ACCESS COURSE…
Tatizo lake lilikuwa kubwa kiasi kwamba, hata kama angekunywa hata chai ilimbidi akimaliza tu ameze pia MAGNESIUM ili kutuliza maumivu na kuondoa gesi tumboni.
Kwahiyo kwa siku walau alimeza Magnesium mara tu hivi!
Kisha akaja pale Ibadani, akalisikia Neno la Mungu, Imani ikaja ndani yake, Nikaweka mikono juu yake halafu YESU KRISTO ALIYE HAI AKAMPONYA!
Kwa miaka zaidi ya 7 alikuwa hawezi kula maharage, pilipili na vyakula kadha wa kadha. Ila sasa anakula kila kitu, na hatumii tena Magnesium wala dawa yoyote…
UAMINI AU USIAMINI, HAITABADILISHA UKWELI YA KUWA YESU YU HAI NA ANATENDA KAZI SASA!
Mimi ni shahidi wa Nguvu na Utendaji wake, nadhibitisha ya kuwa Yesu wa Nazareth yu hai jana, leo na hata milele (Waebrania 13:8)!
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »