MANTLES AND TRANSFER(VYA KIUNGU NA KUSAMBAA/ KUHAMISHIKA KWAKE)

MANTLES AND TRANSFER
(VYA KIUNGU NA KUSAMBAA/ KUHAMISHIKA KWAKE)

Pichani ni Apostle Joshua Selman Nimnak na Bishop Dickson Cornel Kabigumila

Apostle Joshua Selman ni picha ya pili niliyonayo ofisini kwangu kati ya zaidi ya 40 za watu ambao tuna mfanano wa neema ambao nitakuwa nikishare hapa mmoja mmoja hadi waishe wote!

MIFANANO YA WATU HAWA WAWILI

  1. Wote wawili ni watu wanaotambua mno nafasi ya mababa wa imani katika nchi, walioaminiwa kuasisi vitu katika mwili (patriarchs), na wenye kutangulizwa na Mungu mbele yetu kabla yetu!
    Ni watu wanaotembea kwenye kanuni ya heshima (principle of honor) na kanuni ya ufuasi na kuwa chini ya (followership and submission).
  2. Ni watu wa mwili wa Kristo, waliokataa kumilikiwa na udhehebu, ukanisa na utaasisi, watu hawa wanaamini kwenye kuujenga mwili mkubwa wa Kristo na kuufanya mwili wa Kristo uwe na nguvu na matokeo na sio taasisi zao tu!
    Wapo kuhakikisha maslahi ya Ufalme na ya mwili wa Kristo yanakuwa ya kwanza kabla ya mengine yote!
  3. Watu hawa wawili wanaheshimu mno ofisi zote tano za kihuduma: Utume, unabii, uchungaji, ualimu na uinjilisti na si baadhi tu ya huduma bali zote tano na wanaziheshimu kwa uwazi na bila kujali wengine watasema au kuonaje!
  4. Ni watu walio na neema kubwa ya kuzalisha na kutengeneza watu wakuu wa Mungu kwenye maeneo mbalimbali ya maisha!
    Anointed and equipped to raise mighty army of able men for Christ and Kingdom sake!
    Hakuna namna utawasikiliza hawa watu na ubaki ulivyo, watakukera, watakuvuruga mpaka uwe mtu mkuu!
  5. Ni watu wa kuzitambua na kuzitumikia neema hadi zigeuke kuwa zao binafsi!
    Watu hawa wawili wakigundua mtu ana neema au kitu wasichonacho, watamwendea, watamtumikia kwa sadaka, muda, kuwa sehemu yake (association) hadi wakamate ile neema na lile vazi.
    Matokeo yake hawa watu wawili wamekusanya neema nyingi na pako tofauti tofauti kwa moyo huu wa kuupambanua mwili wa Kristo na wenye wasicho nacho!
  6. Watu hawa wawili wote wametoka chini kwa kuziheshimu kanuni za Neno na kanuni zinazotawala maisha wakiwa hawana kitu na hawajulikani na yeyote hadi kufika mahali kila mtu anadai wanayo hekima ya ajabu ya Mungu iletayo masuluhisho!
  7. Watu hawa wawili wamejikita mno kuliamsha kanisa, kukiamsha kizazi cha vijana, kuweka misingi ya wengi kufika juu bila kubahatisha, kwa sababu hakuna bahati kwenye ukuu!
  8. Watu hawa wawili ni watu wa Neno kwelikweli, watu wa karama za Roho kwelikweli, na watu wa kuziheshimu kanuni mno!
  9. Watu hawa wawili ni mfano kwenye kujitoa wao wenyewe, kutoa mali na vitu kwa BWANA na injili, na kutoa muda wao mwingi kwa ajili ya kazi ya Ufalme!

KESHO NITAKULETEA PICHA YA TATU NILIYONAYO OFISINI YA WATU AMBAO NIMEFAIDIKA NA NEEMA ZAO AU TUNASHARE NEEMA FULANI FULANI…
Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
14.02.2024

Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »