MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 3]- JULAI 2019

KUMZALIA MUNGU MATUNDA KWA MIEZI SITA IJAYO

Utangulizi

Mungu amemuumba kila mwanadamu ili AWE MTI WAKE UNAOZAA MATUNDA NA KUPITIA UZALISHAJI HUO YEYE MUNGU APATE KUTUKUZWA (Isaya 61:3).

Ndio maana wakati wa uumbaji, BARAKA ALIYOONA INAMFAA MTU ni KUZAA NA KUONGEZEKA NA KUIJAZA NCHI (Mwanzo 1:28).

Baba wa mbinguni ANATUKUZWA KWA VILE TUNAVYOZAA SANA NA KAMA HATUZAI MATUNDA, NI WAZI YA KUWA HATUKUZWI BALI JINA LAKE LINATUKANWA KUPITIA UTASA UNAOONEKANA MAISHANI MWETU (Yohana 15:8).

Ndiyo maana UTASIKIA YESU AKISEMA, “Kila TAWI LIZAALO MATUNDA HUSAFISHWA SANA, na lile tawi lisilozaa matunda HUKATWA NA KUTUPWA”* (Yohana 15:2).

Anamaanisha ya kuwa KIWANGO CHAKO CHA KUMZALIA MUNGU MATUNDA, KITAAMUA KIWANGO CHA MUNGU KUKUHUDUMIA NA KUKUTUNZA!

Lakini hata kiwango cha KUJIBIWA MAOMBI YAKO NA MUNGU kinategemea kiwango chako cha KUZAA MATUNDA (Yohana 15:7).

Wito mkubwa wa Bwana Yesu kwangu na kwako ni ZAENI MATUNDA YAPASAYO TOBA (Mathayo 3:8).

MATUNDA yapasayo toba ni MFUMO WA MAISHA UNAOTHIBITISHA KWA ULIMWENGU YA KUWA SISI TUMEOKOKA NA YA KUWA YESU ANAKAA NDANI YETU!

NJIA ZA KUMZALIA MUNGU MATUNDA;

1. Matendo yetu ya kila siku
(Mathayo 5:16).

Kupitia matendo yetu JAMII ILIYOTUZUNGUKA INAPASWA IMTUKUZE BABA YETU ALIYE MBINGUNI!
Maisha ya mtu aliyeokoka ni BARUA INAYOSOMWA NA WATU WOTE (2Wakorintho 3:1-3).
Kadri unavyodumu kutenda matendo sahihi na mema, UNAMFUNUA KRISTO NA TABIA YAKE KWA ULIMWENGU, NA KWA NJIA HIYO UNAKUWA UMEZAA MATUNDA!

2. Kuishindania imani uliyopewa na kupiga vita vizuri vya imani
(Yuda 1:3, 1Timotheo 6:12).

Unaposimama DHIDI ya maneno, upinzani na kila kinachotaka UIACHE IMANI YAKO KWA YESU, na kuilinda imani kwa gharama zote, HILO NALO NI TUNDA UNALOKUWA UMEZAA ambalo JAMII itaona na kukiri ya kuwa WEWE SI WA ULIMWENGU HUU NA NI MTU AMBAYE NI MPITAJI NA MSAFIRI DUNIANI, AMBAYE WENYEJI WAKE NI MBINGUNI!
Kwa KUTUNZA huko ushuhuda, UNAKUWA UMEMZALIA MUNGU MATUNDA!

3. Kwa kutumika kwenye nyumba ya Mungu, kwa nguvu, muda, kwa fedha zako, ujuzi wako na kuhakikisha UFALME WA MUNGU UNAJENGWA.
(1Wakorintho 15:58).

Maandiko yanasema TUSIACHE KUYAFANYA HAYO, MAANA TAABU YETU KATIKA BWANA SI BURE (INA malipo na ujira toka kwa BWANA)!

Kila unapotumika kwa ujuzi, muda, nguvu, fedha nakadhalika kwa ajili ya KUUJENGA AU KUUSAMBAZA UFALME WA MUNGU, unakuwa UMEMZALIA MUNGU MATUNDA!

4. Unapohubiri INJILI na kuleta wengine kwa BWANA YESU
(Luka 5:10-11).

Kila anayevuna roho za watu kupitia kuhubiri habari za Yesu na kushirikisha wengine upendo wa Mungu uliotupa wokovu, HUYU MTU NI MTU BORA AZAAYE MATUNDA KWENYE UFALME WA MUNGU NA KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU!

Mungu hapendi hata mmoja apotee bali WOTE WAIFIKIE TOBA (2Petro 3:8-9).
Hivyo unapomshuhudia mtu habari za Yesu, hata asipookoka papo hapo, UNAKUWA MTI UZAAO MBELE ZA MUNGU!
Na mtu huyo AKIKUBALI NA KUIAMINI INJILI YA YESU, UNAKUWA UMEZAA TUNDA KWA AJILI YA KRISTO YESU!

5. Tunda la Roho
(Wagalatia 5:22-23).
Tunda la Roho ni tunda linalothibitisha UWEPO WA ROHO WA MUNGU NDANI YA MWAMINI!
Kadri linavyoonekana maishani mwa mtu, MTU HUYU ANAKUWA NI MTU AMBAYE ANAZAA MATUNDA YAPASAYO TOBA!

MAOMBI

ASUBUHI

Muombe Mungu AKUSAFISHE NA KUKUTENGENEZA, ILI UWEZE KUMZALIA MATUNDA YAPASAYO TOBA (Yohana 15:2, Mathayo 3:8).
Muombe Mungu, AONDOE NDANI YAKO KILA TABIA, MWENENDO, NA MFUMO WA MAISHA UNAOKUZUIA USIWE MTU MWENYE MATUNDA MBELE ZA MUNGU!

MCHANA

OMBI
Muombe Mungu akupe nguvu na ujasiri wa KUWAFIKIA WATU WENGI KWA HABARI NJEMA ZA YESU NA KUWALETA KWAKE kama alivyofanya MWANAMKE MSAMARIA ALIPOLETA MJI MZIMA KWA YESU (Yohana 4:28-29).
Muombe Mungu AKUPE UJASIRI KAMA SIMBA, UWEZE KUIHUBIRI INJILI NA KULETA WATU WENGI KWAKE KAMA PETRO (Matendo 2:5-39)!

Muombe Mungu AKUPE KUWAPELEKEA WENGINE HABARI NJEMA ZA KUWAPATANISHA NA MUNGU (2Wakorintho 5:18-20).

JIONI

*”KAMA MKIKUBALI NA KUMTUMIKIA, MTAPISHA SIKU ZENU KATIKA FURAHA NA MIAKA YENU KATIKA KUFANIKIWA”*
(Ayubu 36:11).

OMBI

Muombe Mungu akupe MOYO WA KUTUMIKA KWAKE KWA UAMINIFU KWA MIEZI YOTE SITA IJAYO, ILI SIKU ZAKO ZOTE KATIKA MIEZI SITA IJAYO ZIWE ZA FURAHA NA KUFANIKIWA!
WALE WANAOMTUMIKIA MUNGU, HAO HUINULIWA, HUTUKUZWA NA KUWA JUU SANA (Isaya 52:13)!

HONGERA KWA KUMALIZA SIKU TATU ZA MFUNGO,
NAAMINI UNABADILISHWA NA KUJENGWA KUPITIA MFUNGO HUU!

WEWE NI WA THAMANI,
WEWE NI JIBU NA SULUHU YA DUNIA YAKO,
TUKUTANE KESHO SIKU YA NNE YA MFUNGO WETU!

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila.
24/07/2019

NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HII, AMBAYO UTAITOA MWISHO WA MFUNGO!

Mawasiliano zaidi:
WhatsApp: 0655 466 675
Tovuti: www.yesunibwana.co.tz
Instagram: @mwalimukabigumila

Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »