MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 8]- JULAI 2019

ULINZI WA MUNGU KWENYE KILA ENEO LA MAISHA YETU KWA MIEZI SITA HII YA MWISHO NA MAISHA YETU YOTE TUWAPO DUNIANI

Utangulizi

Mungu anapenda tuwe salama kabisa mbali na kila shambulizi au hatari toka kwa adui Shetani, matukio mabaya, maradhi na magonjwa na kila kinachotishia kuhatarisha maisha yetu!

Kuthibitisha hili, Mungu anasema ATATULINDA KULIKO MWANAMKE AMLINDAVYO MWANAE WA KUMZAA, AMEKUCHORA KWENYE VITANGA VYA MIKONO YAKE ILI AWE ANA MONITOR MAISHA YAKO KILA DAKIKA KAMA VILE WATU WALINDAVYO NYUMBA ZAO KWA KAMERA MAALUM ZA USALAMA (Isaya 49:14-16)!

Kama haitoshi anasema, ATAKUWA UKUTA WA MOTO KUKUZUNGUKA PANDE ZOTE (HUDUMA, FAMILIA, KAZI ZAKO NA KILA ENEO LA MAISHA YAKO), NA KILA ATAKAYEJARIBU KUKUGUSA ATAKUWA AMEIGUSA MBONI YA JICHO LAKE (Zekaria 2:5, Zekaria 2:8).

Kwa namna ambavyo anataka ustawi na kufanikiwa, ANA KIKOSI MAALUM CHA MALAIKA WA KUKUONGOZA MPAKA UFIKIE PALE ALIPOKUKUSUDIA KIMAISHA, AMBAO WATAKULINDA KATIKA NJIA YAKO YA KUELEKEA MAFANIKIO (Kutoka 23:20).

Hivyo nataka ujue yakini ya kuwa Mungu HATAKI ushambuliwe, uteswe wala uonewe kamwe na Shetani au namna yoyote ya utesi!

Hivyo inua viwango vyako vya kukubali ukweli huu, na kamata kila NENO LA ULINZI UTAKALOLIPATA KATIKA UJUMBE HUU, NA USILIACHIE KOMAA NALO MPAKA LIZAE ULINZI MAISHANI MWAKO!

MUNGU ANALINDA WATU WAKE KWA NJIA ZIFUATAZO;

1. Yeye MWENYEWE ni mlinzi wa WATU wake, asiye lala wala kusinzia (Zaburi 121:3-8).
•Ni mlinzi pekee asiyesinzia wala kulala
•Atazuia JUA lisikupe wala MWEZI maana yake atazuia shambulizi lolote, liwe limekuja mchana (jua) au limekuja usiku (mwezi)!
•Ni mlinzi pekee anayeweza KUKULINDA NA MABAYA YOTE/ YA NAMNA ZOTE (Shetani, DHAMBI, Magonjwa, Umasikini, Kuharibika Kwa ndoa na familia, Kazi nakadhalika)!

ii) JINA LA YESU
Kuna ulinzi ndani ya jina la Yesu, hata Yesu MWENYEWE alilitumia kuwalinda wanafunzi wake! Na akasema litatumika kutulinda na sisi TUTAKAOMUAMINI KUPITIA INJILI YAKE ITAKAYOHUBIRIWA NA MITUME (Yohana 17:11-20).

iii) KULINDWA KWA NGUVU ZA MUNGU KWA NJIA YA IMANI
Tunalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya IMANI (1Petro 1:5).
Imani ni ngao ambayo Inaweza KUZIMA KILA MSHALE WA MOTO WA YULE ADUI (Waefeso 6:16-17).
NI WAJIBU WETU KUHAKIKISHA IMANI ZETU ZIMEJENGWA NA KUWA IMARA MUDA WOTE KWA NENO LA MUNGU LA VIWANGO!

iv) KUPITIA MALAIKA ZAKE
Mungu hulinda watu wake kupitia jeshi lake la malaika (Kutoka 23:20, Zaburi 34:7, Zaburi 91:10-11).

v) BWANA YESU ANAWEZA KUTULINDA TUSIJIKWAE HATA SIKU ILE YA MWISHO AJAPO.
Yuda 1:24-25

vi) MAOMBI YANAWEZA KUWEKA HAYO MATANO JUU KUFANYA KAZI YA ULINZI
(Zaburi 32:6, Mathayo 26:40-44).

vii) MIMI NA WEWE TUNAPOLITII NENO LA KRISTO NA KUTOLETA UTANI NA DHAMBI NA DUNIA, TUNAKUWA TUMEJILINDA/ TUMEJIHAKIKISHIA USALAMA.
1Yohana 5:18, 1Timotheo 4:16

viii) UNAPOKUWA ACTIVE ROHONI, YAANI ROHO YAKO IKO HAI, HUO NI ULINZI
Mathayo 13:25-30, 1Petro 5:8-10, Ufunuo 3:10
Hakikisha haupoi wala KUFA kiroho, huo ni ulinzi wa muhimu sana DHIDI ya kila shambulizi na uonevu wa SHETANI.
Mtu ambaye YUKO HAI ROHONI, HAJAANGUKA KWENYE DHAMBI NA DUNIA, ANAKUWA NA ULINZI WA AJABU MNO!
Ilinde roho yako, ili uwe salama.

MAMBO AMBAYO MUNGU ANATULINDA DHIDI YAKE:

1. Shetani
Ufunuo 12:10-17, 1Petro 5:8

2. DHAMBI
Yuda 1:24, 1Yohana 5:18

3. MAADUI ZETU WANADAMU WAOVU
Zaburi 60:12, Waebrania 13:6

4. HILA NA MITEGO ILIYOKO MBELE (SNARES IN FUTURE)
Zaburi 32:6, Zaburi 35:1-28

5. MAUTI NA KIFO
Zaburi 68:20, Hosea 13:14

MAOMBI YA LEO

OMBEA MAENEO YOTE AMBAYO YANAHITAJI ULINZI WA MUNGU:

1. AFYA
2. IMANI YAKO ISIHARIBIWE WALA KUPUNGUA
3. FAMILIA YAKO NA NDOA KWA WALE WALIOOA NA KUOLEWA
4. UCHUMI WAKO
5. HUDUMA YAKO/ UTUMISHI WAKO
6. TAIFA LETU

MUNGU AKUBARIKI KWA KUWEZA KUOMBA NA KUFUNGA LEO SIKU YA NANE,
TUKUTANE KESHO SIKU YA TISA.

WEWE NI WA THAMANI,
WEWE NI MBARIKIWA,
WEWE NI SULUHU YA WENGI.

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila,
29/07/2019.

 

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »