MFUNGO WA SIKU 10 WA MWISHO WA MWEZI [SIKU YA TANO]

NGUVU YA MANENO

Maandiko:

“Mimi, Bwana, NINAYAUMBA MATUNDA YA MIDOMO (kinachozaliwa mdomoni ni maneno)…”
(Isaya 57:19).

“Waambieni, Kama niishivyo, asema Bwana, HAKIKA YANGU KAMA NINYI MLIVYONENA MASIKIONI MWANGU, NDIVYO NITAKAVYOWAFANYIA NINYI”
(Hesabu 14:28).

“Tumbo la mtu (maisha ya mtu) litajazwa MATUNDA YA KINYWA CHAKE; Atashiba MAZAO YA MIDOMO YAKE”
(Mithali 18:20).

“MAUTI NA UZIMA huwa katika UWEZO WA ULIMI; Na wao waupendao watakula matunda yake”
(Mithali 18:21).

“NAO ULIMI NI MOTO;…”
(Yakobo 3:6).

“…ULIMI…NI UOVU USIOTULIA, UMEJAA SUMU ILETAYO MAUTI”
(Yakobo 3:8).

UKWELI KUHUSU MANENO

1. Maneno yanaweza kuachilia nguvu mojawapo kati ya uzima au mauti (Mithali 18:21)

2. Maneno yanaweza kuamua Mungu afanye nini maishani mwa mtu (Hesabu 14:28)

3. Maneno yanaweza kubeba nguvu ya baraka au laana (Mwanzo 1:28, Yakobo 3:9-10).

4. Maneno yanaweza kubeba nguvu ya kumnasa na kumfunga mtu (Mithali 6:2).

5. Maneno yanaweza kubeba imani ya mtu (2Wakorintho 4:13-14, Marko 11:23).

6. Maneno yana nguvu ya kuleta amani au kuchochea ugomvi (Mithali 26:20).

7. Maneno yana nguvu ya kukupa haki au hukumu toka kwa Mungu (Mathayo 12:36-37).

8. Maneno ni ushahidi au kipimo cha kujua yaliyojificha moyoni mwa mtu (Mathayo 12:34).

9. Maneno yako yanaweza kuleta malaika maishani mwako au kuwafukuza (Danieli 10:12)

10. Maneno yako yanaweza kuamua nini kitakachotokea maishani mwako (Isaya 57:19).

11. Maneno yako yanaweza kujaa Neema au uovu kutegemea HAZINA ULIYOJAZA MOYONI (Wakolosai 4:6, Waefeso 4:29, Mathayo 12:33-34).

MAOMBI

ASUBUHI

1. Muombe Mungu;

i) Ayaharibu maisha na kila tukio lisilo jema ambayo uliyatamka na Mungu AKAYAUMBA (Mithali 6:2).

ii) Adhihirishe KILA JEMA ULILOTAMKA KWENYE MAISHA YAKO NA AKALIUMBA.
(Isaya 57:19).

2. Muombe Mungu;

i) Aghairi kila baya alilokuwa AMEFANYA kwako, familia, watoto, mmeo kwa sababu VILE ULIVYOSEMA NDIVYO ALIVYOFANYA.

ii) Muombe Mungu AFANYE KILA JEMA NA LA BARAKA ULILOSEMA MASIKIONI MWAKE kwa habari ya maisha yako, familia yako, kazi, biashara, huduma nakadhalika.
(Hesabu 14:28).

3. Muombe Mungu;

i)Aondoe KILA MAUTI uliyokuwa umeiumba kwa mdomo wako.

ii) Adhirishe KILA UZIMA kwenye kila jambo ulilolitamkia maneno ya uzima.
(Mithali 18:21).

MCHANA

4. Muombe Mungu;

i) Aondoe KILA MTI WA UOVU ULIOUOTESHA KWA MANENO YAKO NA UNAZAA MATUNDA MAOVU kwako na watu wako.

ii) Atunze KILA MTI MWEMA ULIOUPANDA KWA MANENO MEMA NA MATUNDA YAKE MEMA yazidi kuonekana kwenye maisha yako na watu wako.
(Mithali 18:20).

JIONI

5. Muombe Roho Mtakatifu;

i) Azime KILA MOTO UNAOTEKETEZA MAISHA YAKO uliouwasha kwa ULIMI wako.

ii) Ahakikishe KILA MOTO ULIOWASHA KUTEKETEZA mapando ya adui, mikakati ya kuzimu na majeshi ya adui KWA ULIMI WAKO, USIZIMIKE Mpaka utakapokwisha kuharibu kila lililo kinyume na mapenzi ya Mungu maishani mwako!
(Yakobo 3:6).

6. Muombe Roho wa Mungu ndani yako aliachilie tunda lake ndani yako, ili uwe na uwezo wa kudhibiti kinywa na ulimi wako (Wagalatia 5:22-23).

NB: Niombe mimi mchungaji Dickson Kabigumila, mke wangu Mercy na watu wa Mungu wa ABC tunaowachunga, MANENO YETU YAKOLEE YAJAE NEEMA NA YAKOLEE MUNYU, NA KILA NENO OVU LISITOKE VINYWANI MWETU (Wakolosai 4:6, Waefeso 4:29).

Tukutane kesho siku ya sita,

Uzidi kutunzwa na Yesu, maana wewe ni wa thamani na umebeba majibu ya dunia yako!

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »