MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -AUGUST [SIKU YA 8]

KUSUDIA/ DHAMIRIA/ AMUA KUMPENDEZA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO YOTE UWAPO DUNIANI.

Utangulizi

Katika Biblia kuna watu ambao Mungu anasema WALIUPENDEZA MOYO WAKE!

Tuwaone baadhi yao kwanza;

1. HABILI (ABEL)
*”…Bwana akamtakabali Habili na Sadaka yake…”* (Mwanzo 4:6).

*”Kwa imani, HABILI alimtolea Mungu sadaka iliyo bora kuliko Kaini; Kwa hiyo alishuhudiwa ya kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, Ijapokuwa amekufa, angali akinena…”* (Waebrania 11:4).

Huyu ni mtu wa kwanza ambaye alimpenda Mungu kiasi cha kuleta WAZAO WA KWANZA WA WANYAMA WAKE/ MALIMBUKO (Mwanzo 4:4).
Na kwa mujibu wa MITHALI 3:9-10, MTU ANAYETOA MALIMBUKO, NI MTU AMBAYE ANA KIWANGO CHA JUU CHA HESHIMA KWA MUNGU!
*”Mheshimu BWANA, kwa MALI YAKO, na kwa MALIMBUKO YA MAZAO YAKO YOTE”*

Mbali ya upendo na heshima aliyokuwa nayo kwa Mungu, kiasi cha KUTOA MALIMBUKO, lakini pia ALITOA SEHEMU ZILIZONONA ZA WANYAMA, ikiwa na maana ALITOA KIKUBWA/ KIZITO kuliko alichobaki nacho!
Alikuwa tayari KUMPA MUNGU KILICHO BORA hata kama yeye atabaki na cha kawaida mno!

Na kwa KANUNI ZA UFALME WA MUNGU… KUTOA NDICHO KIWANGO CHA JUU CHA KUTHIBITISHA UPENDO WAKO KWA MUNGU!

Ibrahimu kipenzi cha Mungu, mbali ya kutembea na Mungu toka akiwa na miaka 75 alipoitwa, akiwa na miaka 116, yaani miaka 41 toka amjue Mungu, ALIPEWA AGIZO LA KUMTOA ISAKA ambaye alikuwa na miaka 16 wakati huo (Mwanzo 22:1-3)!

Alipotii na kumtoa mzaliwa wake wa pekee, KITENDO KILE KILIMSHANGAZA HATA MUNGU MWENYEWE, maana tangia hapo hakukuwa na MTU aliyewahi KUONESHA UPENDO WA VITENDO KWA MUNGU KUFIKIA KIWANGO KILE (Mwanzo 22:15-18)!

Utagundua, KUMPENDA MUNGU SI MANENO MATUPU! Kumpenda Mungu si NYIMBO kama wengi wetu tunavyoishia KUIMBA TUNAMPENDA!
Kumpenda Mungu ni KUJAWA NA HESHIMA KWAKE, INAYOKUFANYA KUTOKUWA NA UWEZO WA KUMNYIMA CHOCHOTE AKIKUGUSA AU AKIKUSEMESHA!

Je unataka kuwa kama HABILI?
Je uko tayari kumpenda Mungu na kumheshimu kwa sadaka zilizonona / bora na MALIMBUKO kama yeye?
Usisahau, Damu ya Yesu inalo agano lililo bora ililotupa kama wana wa Mungu kwa imani kila mmoja aliyemkubali na kumpokea (Yohana 1:12), lakini kuna walioamua NDANI YA AGANO HILI LILILO BORA KUMPENDA NA KUWA TAYARI KUFANYA CHOCHOTE KWA AJILI YA KRISTO NA INJILI hata kutoa CHOCHOTE KWAKE bila maswali, kwa vile tu PENDO LA MUNGU NDANI YAO limewapa KUMPENDA KWA MIOYO YAO YOTE, NA HAWAWEZI KUMNYIMA MUNGU CHOCHOTE!
Hawa ndio wale ambao Mungu huingia nao agano binafsi, nje ya agano lililo bora la msalaba ambalo ni la wote! Kila mtu ambaye ni MTOAJI WA DHATI TOKA MOYONI, analo agano binafsi na Mungu, maana Maandiko hayatanguki (Zaburi 50:5)!

Miezi MINNE hiii ijayo, amua kuingia VIWANGO hivi vya kipekee, na maisha yako yote yaliyosalia, DHIHIRISHA IMANI YAKO KWA MATENDO KAMA HABILI!
*”…KWA IMANI… HABILI… ALIMTOLEA MUNGU… SADAKA ILIYO BORA…”* (Waebrania 11:4, nimeachanisha maneno haya walau uweze kuona uzito wa moja moja).

*KWA IMANI*
Imani ya kweli itakufanya uambatanishe na matendo ya imani, mojawapo likiwa kumtolea Mungu kwa ubora kama ishara ya upendo ulionao!

*HABILI*
Halikuwa jambo la kila mtu, na hata sasa si kila mtu ambaye jambo hili litapenya MOYONI mwake!
HABILI alipata Ufunuo binafsi, ambao Kaini hakuupata!
HABILI alipata Ufunuo ambao baba yake Adamu na mama yake Eva hawakuupata!

Mungu akujalie KUWA HABILI toka leo bila kujali wangapi hawajafunuliwa jambo hili wanaokuzunguka au kupinga!
Ifikie mahali, kama ingeandikwa Biblia nyingine, tungeona pia mahali ambako panasema, *”…Kwa imani Dickson alimtolea Mungu sadaka bora…”*
Dhamiria iandikwe hivyo MBINGUNI kwenye KITABU cha matendo ya WATAKATIFU wa kizazi chetu, kwa habari ya maisha yako, KAMA AMBAVYO SADAKA NA MAOMBI YA KORNELIO VILIKUWA UKUMBUSHO/ VILIWEKA REKODI, HATA MUNGU KUMTUMIA PETRO AMWAMBIE HABARI NJEMA ZA WOKOVU (Matendo 10:1-3).

Kumbuka hili: *KUOKOKA HAKUJATUNYANG’ANYA WAJIBU HUU WA KUUPENDEZA MOYO WA MWOKOZI WETU, INGAWA ALITUPENDA TUNGALI WAOVU NA WASIOSTAHILI! MTU ASIYEKUAMBIA HILI, AKIDAI LIMEMALIZWA NA MSALABA, HUYO NI MTU ASIYEKUTAKIA MEMA WEWE NA UCHUMI WAKO!*

2. NUHU

*”…LAKINI NUHU AKAPATA NEEMA MACHONI PA BWANA… “*
(Mwanzo 6:8).
Huyu ni mtu aliyepata kibali maalum cha kuepuka adhabu ya gharika iliyouteketeza ULIMWENGU wa Wakati ule!
Mbali ya kukaa na kuzungukwa na watu waovu, ALISIMAMIA VIWANGO VYA UTAKATIFU NA UKAMILIFU BILA KULEGEZA KAMBA AU KUTAFUTA MBINU NA MAANDIKO YA KUMPA UHALALI WA KUTENDA DHAMBI (HE DIDN’T COMPROMISE THE STANDARDS)!

NUHU atawahukumu wengi waliookoka SIKU ile ya mwisho!
Hatuna tofauti kubwa ya mambo yaliyokuwepo wakati wa NUHU na yaliyoko sasa wakati huu.
Na wengi waliookoka WAMEAMUA KUSHUSHA NA KULEGEZA VIWANGO wakidai WAKO CHINI YA NEEMA, hivyo wanautumia Uhuru wao ndani ya Kristo KUISHI OVYO OVYO, NA KUIFUATISHA NAMNA YA DUNIA HII!
NUHU alitembea na Mungu, HAKUTUMIA VIBAYA NEEMA ALIYOKUWA NAYO, ALIITUMIA KUTEMBEA MBALI NA DHAMBI TOFAUTI NA WENGI WETU TUNAVYOITUMIA KAMA KICHAKA CHA KUFICHIA DHAMBI NA UCHAFU!
Neema ya Kweli, NI MWALIMU, inatufundisha KUUKATAA UBAYA WA KILA NAMNA, NA KUISHI MAISHA YA HAKI, KIASI NA UTAUWA KATIKA ULIMWENGU HUU WA SASA ULIOCHAFUKA AMBAO HATA WALIOKO MAKANISANI WANAPUYANGA KWENYE DHAMBI (Tito 2:11-12)!

Ni maombi yangu kwa Mungu, mimi na wewe tuvuke, tutoke mahali pa kujificha dhambini kwa kisingizio cha uwepo wa neema, Bali TUZAE MATUNDA YA NEEMA AMBAYO NI HAKI, KIASI NA UTAUWA tena katika ULIMWENGU HUU WA SASA!

3. HENOKO
*”Henoko AKATEMBEA PAMOJA NA MUNGU, NAYE AKATOWEKA, MAANA MUNGU ALIMTWAA”*
(Mwanzo 5:24).

*”Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; Maana, KABLA YA KUHAMISHWA alikuwa ameshuhudiwa kwamba AMEMPENDEZA MUNGU”*
(Waebrania 11:5).

Sijui kama umegundua niliyoona mimi hapo JUU!
-Henoko ni mtu ambaye si kwamba alizijua habari za Mungu, si tu alimuamini Mungu, bali ALITEMBEA PAMOJA NA MUNGU!

-Henoko HAKUFA, bali ALIHAMISHWA TOKA DUNIANI KWENDA MBINGUNI MZIMA MZIMA kama Eliya, tena yeye hakufuatwa na gari la moto, ALIFUATWA NA MUNGU MWENYEWE ALIYEKUWA AMEMPENDEZA SANA!

-Akiwa bado hapa duniani, si baada ya KUFA au kutwaliwa, HATA USHUHUDA WAKE KWA WATU WOTE WALIOISHI PAMOJA NAYE, walishuhudia ya kuwa ALIKUWA AMEMPEDEZA MUNGU! Yaani jamii yake, mke wake, watoto wake, WOTE WALISHUHUDIA WAZIWAZI YA KUWA MTU HUYU NI KIPENZI CHA MUNGU!

Je nawe umedhamiria ushuhuda wako uwe upi?
Utaitwa ANAYEMPENDEZA MUNGU au ANAYEMHUZUNISHA MUNGU?
Utaitwa KIPENZI CHA MUNGU au MVUNJA MOYO WA MUNGU kama walivyokuwa watu wa wakati a NUHU au wenyeji wa Sodoma na Gomora?
Uamuzi uko mikononi mwako, wewe ndiye utakayeamua, na UKIAMUA kwa DHATI kabisa, *NURU ITAKUANGAZIA NA NJIA YAKO ITAKUWA HERI NA SALAMA* na USAFI WA MIKONO YAKO utakupa kuishi salama (Ayubu 22:28-30)!

4. AYUBU

*”…Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! UMEMWANGALIA HUYO MTUMISHI WANGU AYUBU? Kwa kuwa HAPANA MMOJA ALIYE KAMA YEYE DUNIANI, MTU MKAMILIFU NA MWELEKEVU, MWENYE KUMCHA MUNGU NA KUEPUKANA NA UOVU…”*
(Ayubu 1:8).

Mungu ana watu mabilioni duniani, lakini kuna baadhi ya watu ambao AMEWAPA SPECIAL CARE!
Ndivyo ilivyokuwa kwa Ayubu.
Ni MTU ALIYEMPENDEZA MUNGU MOYO WAKE!
Alikuwa ni mtu ALIYEJAA MNO KWENYE MOYO WA MUNGU, ANAYEMUWAZA NA KUMUULIZIA KIMAALUM TENA KWA JINA LAKE!

Naamini unatamani kuwa na special place kwenye akili, moyo na mawazo ya Mungu, sivyo?
Jibu ni rahisi amua tu kwa neema ya Mungu kuishi alivyoishi Ayubu!

Ayubu alikuwaje?
-Mtu mkamilifu
-Mtu mwelekevu (anayeelezeka)
-Mtu mcha Mungu
-Mtu anayeepuka uovu kwa makusudi
(Ayubu 1:3, Ayubu 1:8).

Ni uamuzi wako kwenye miezi hii SITA ijayo, uwe kama Ayubu au la!
Hilo liko ndani ya uamuzi wako!

5. YUSUFU
*”…NITENDEJE UOVU HUU MKUBWA NIMKOSE MUNGU?”*
(Mwanzo 39:1-9).

-Alikuwa na nidhamu binafsi ya kutomtenda Mungu DHAMBI hata kama hakuna anayeona au atakayejua

-Hakuogopa kutenda DHAMBI kwa sababu ya uwepo wa Jehanamu, bali kwa vile HATAKI KUUPOTEZA UWEPO WA MUNGU MAISHANI MWAKE

-Hakuogopa kutenda DHAMBI kwa kuogopa dunia itamsema au kumcheka, bali MUNGU AONAYE SIRINI HATAFURAHISHWA

Na kwa sababu ya COMMITMENT KUBWA KIASI HIKI, Yusufu ALIKUWA NA IMPACT YA KIWANGO CHA KUTISHA!

Uamuzi unabaki mikononi mwako, hata Mungu hawezi kukulazimisha au kukushikia fimbo, AMUA LEO KUANZA UPYA NA KUWA KIPENZI CHA MUNGU!

6. DANIELI

*”… NAYE DANIELI… ALIADHIMIA MOYONI MWAKE (ALIFANYA UAMUZI BINAFSI), YA KUWA HATAJITIA UNAJISI…”*
(Danieli 1:8).
Huyu ni mtu kipenzi cha Mungu ambaye HATA SIMBA HAWAKUWEZA KUFUNGUA MDOMO KUMLA, BALI MALAIKA WALIMLINDA NA KUFUNGA VINYWA VYAO ASIGUSWE (Danieli 6)!

-Huyu ni mtu ambaye KUTOKANA NA MAISHA YAKE YA KUJITENGA NA KUTOJITIA UNAJISI, Mungu aliamua kumpa AKILI BORA, ROHO WAKE, NA KUMTOFAUTISHA (Danieli 1:17-18, Danieli 5:10-14)!
-Ni mtu ambaye ALIKUWA KWENYE SERIKALI TATU TOFAUTI ZA WAFALME WA BABELI KAMA WAZIRI MKUU, tangia Nebukadneza, Betshaza na Dario (Danieli 1 hadi Danieli 6 utaona)!
HE WAS A MAN OF ENDLESS IMPACT!

HABARI NJEMA;

Kila mmoja wetu amekusudiwa kuwa *CHOMBO CHA HESHIMA, CHA THAMANI, KIMFAACHO MUNGU KWA KILA KAZI NJEMA* lakini lazima ufanye uamuzi wako binafsi wa *KUJITAKASA/ KUGEUZA MAISHA YAKO* kwa *KUJITENGA NA WATU, VITU, TABIA NA MIFUMO YA MAISHA* inayokula UTUKUFU NA THAMANI KUBWA ULIYONAYO!

NA HILI NDILO LITAKUWA OMBI LETU KUU!

ANDIKO LA KUSIMAMIA: 2Timotheo 2:19-21

VYA KUOMBEA

-Kuwa muwazi MBELE ZA MUNGU, mueleze maeneo ambayo bado unakwama, na omba NEEMA NA NGUVU YA KUVUKA JUMLA (Ombea hili kwa walau dk 30).

-Omba kwa kadri ya uliyoona kwenye maisha ya WALIOMPENDEZA MUNGU, YALE UNAYOTAKA BWANA AKUIMARISHE ILI UMPENDEZE KWELI KWELI (Omba walau Dk. 30).

-Mwisho kabisa mshukuru Mungu kwa mfungo wa SIKU hizi KUMI na miezi MINNE ijayo ya BARAKA NA USTAWI (Zaburi 92:1).
Niombee mimi, familia yangu na huduma ya ABC kwa kadri unavyoguswa na maisha NA HUDUMA hii!

WEWE NI MBARIKIWA,
WEWE NI SULUHU KWA DUNIA YAKO,
WEWE NI JIBU LA MAMILIONI YA WATU!

TUKUTANE KESHO, SIKU YA TISA

MAELEKEZO: *ZITUMIE PRAYER POINTS ZA SIKU HIZI KUMI KAMA MUONGOZO WA MAISHA YAKO KWA MIEZI MINNE ILIYOKO MBELE YAKO, YAISHI NAWE UTAJAA SHUHUDA!*

*SADAKA MAALUM YA MFUNGO KWA KADRI ULIVYOGUSWA, NA KWA VILE UNAVYOJALIWA, UNAWEZA KUITUMA UIPATAPO, KWENYE MOJA YA NJIA HIZI CHINI;*

TUMA SADAKA HIYO:
M-PESA: 0753 466 675
TIGOPESA: 0655 466 675
CRDB: 01J 2084559100 (DICKSON CORNEL KABIGUMILA)

Ni mimi ndugu yako,
Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,

MAWASILIANO ZAIDI:
Tovuti: www.yesunibwana.co.tz

Instagram: @mwalimukabigumila

Facebook: MWALIMU DICKSON CORNEL KABIGUMILA

WhatsApp: 0655 466 675

YouTube:

*PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA*

NA

*CHURCH STATION*

Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »