MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -AUGUST [SIKU YA 9]

NGUVU YA KUCHUKUA HATUA (THE POWER OF TAKING A STEP).

Maandiko:

“Wakati HATUA ZANGU zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali lilipomimina mito ya maziwa”
(Ayubu 29:6).

“Je yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu HATUA zangu zote?”
(Ayubu 31:4).

“Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, HATUA ZANGU hazikuondoshwa”
(Zaburi 17:5).

“Umezifanyia nafasi HATUA ZANGU, na miguu yangu haikuteleza”
(Zaburi 18:36).

“HATUA ZA MTU zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake”
(Zaburi 37:23).

“Akanipandisha toka shimo la uharibifu, toka udongo wa utelezi; akaisimamisha miguu yangu mwambani, akaziimarisha HATUA zangu”
(Zaburi 40:2).

“Uzielekeze HATUA ZANGU kwa Neno lako, Uovu usije ukanimiliki”
(Zaburi 119:133).

“Ee Bwana, unilinde na mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na mtu wa jeuri; Waliowaza kuzipotosha HATUA ZANGU”
(Zaburi 140:4).

“Uendapo, HATUA ZAKO hazitadhihikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa”
(Mithali 4:12).

“Moyo wa mtu hufikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza HATUA ZAKE”
(Mithali 16:9).

” Ee Bwana, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza HATUA ZAKE si katika uwezo wa mwanadamu”
(Yeremia 10:23).

MAMBO YA KUJIFUNZA KUHUSU KUCHUKUA HATUA;

1. Kila kitu kinabaki katika hali hiyohiyo mpaka mtu achukue HATUA kugeuza hilo jambo!

2. Kila historia iliyowahi kuandikwa, mbaya au nzuri ni matokeo ya HATUA nzuri au mbaya!

3. Mungu ameturuhusu kupanga mipango (njia), lakini anataka tumshirikishe ili aongoze HATUA zetu!

4. Kila safari ndefu, Mungu ameweka utaratibu igawanyike katika HATUA moja moja!

5. Kila jengo refu linapandwa kwa HATUA moja moja!

6. Hatua si safari, lakini safari ni HATUA!
Ukipiga hatua moja haikufanyi ufike mwisho wa safari, lakini safari yoyote ni matokeo ya hatua moja moja nyingi!

7. Maisha ni hatua, ukiridhika na ulipo, kesho ikija utakuwa umepitwa na muda.
Waangalie mashirika ya simu za mezani na shirika la posta, wamechelewa kupiga hatua, na muda umewapita!
Ili uendelee kubaki RELEVANT kwenye dunia yako, lazima uendelee KUPIGA HATUA kila siku!

BAADHI YA WATU WALIOCHUKUA HATUA KWENYE BIBLIA;

1. Nuhu alichukua hatua kujenga Safina bila kusubiri mvua inyeshe kwanza!
“Wakati mwingine huhitaji kuona kila kitu ili uchukue hatua, UKISHAONA KATIKA BIBLIA YAKO au kuambiwa ndani na Roho Mtakatifu, CHUKUA HATUA MOJA UNAYOIONA, mwanga mkubwa utaupata kadri unavyosogea”

2. Musa alichukua HATUA ya imani kwenda Misri mahali anapotafutwa kwa kosa la kuua ili awe mkombozi, hakuwa na picha nzima, alikuwa na fimbo na mkono wake ambao unaweza kuwa na ukoma na maneno machache aliyopewa na Mungu. Miujiza mingine tisa ilitokea huko huko na hakuwa akiijua kabla… Anzia hapo unapoona, mengine utakutana nayo njiani”

3. Rahabu kahaba ALICHUKUA HATUA YA IMANI kuwakaribisha Wapelezi waliotumwa na Yoshua na akapona yeye na ndugu zake… Hakuona mwisho wake lakini ALICHUKUA HATUA aliyoona, Mungu akamalizia kilichobakia”

4. Mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka kumi na miwili, baada ya KUSIKIA HABARI ZA YESU, ALICHUKUA HATUA YA KUGUSA PINDO LA VAZI LAKE, na Mungu akamalizia kisichoonekana!
“Anza na hatua moja unayoiona muache Mungu afanye usiyoyaona unayoyatarajia”

MAOMBI

Asubuhi

1. Omba Mungu akupe moyo wa ujasiri wa kuchukua hatua kuelekea kwenye ndoto uliyonayo!
(Marko 5:25-34, 2Wafalme 7:3- 9).

2. Omba Mungu aziongoze hatua zako na kuzithibitisha, ili kila ufanyalo likamilike na kufanikiwa.
(Zaburi 37:5-6, 23-26).

Mchana

1. Omba dhidi ya kila watu wanaokwamisha hatua zako na wanaotaka kukuangusha, Mungu awashughulikie.
(Zaburi 17:11, Zaburi 140:4).

2. Muombe Mungu akupe hatua chanya, zinazoelekea mafanikio na utimilifu wa maono na ndoto zako kila iitwapo leo.
(Mithali 4:18-19, Zaburi 92:12-15).

Jioni

1. Omba lolote utakalo Bwana Yesu akutendee leo.
(Luka 18:41-42, Hosea 6:1-4).

2. Niombee mimi Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila.
(Isaya 52:13, Zaburi 89:20-37).

3. Mshukuru Mungu kwa kujibu kila ombi tuliloomba leo.
(Yohana 14:13-14, Isaya 65:24).

Tukutane kesho Jumamosi siku ya kumi, tuhitimishe pamoja!
Umebarikiwa sana,
Umebeba majibu ya mamilioni,

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji mwanzilishi,
ABC GLOBAL.

USIACHE KUFUATILIA TOVUTI YANGU YA:
www.yesunibwana.co.tz

YOUTUBE:
TAFUTA CHANNEL HIZI

CHURCH STATION
&
PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA

INSTAGRAM:
@MWALIMUKABIGUMILA

NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YAKO YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU KAMA UNAVYOGUSWA MOYONI KWA MOYO WA KUPENDA, NA KADRI MUNGU ALIVYOKUFANIKISHA! KAMA UNAYO TAYARI, WAWEZA KUTUMA KWENYE:

M-PESA: 0753 466 675
TIGOPESA: 0655 466 675

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »