MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 8]

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE.
https://i0.wp.com/cdn.charismanews.com/images/stories/2014/opinion/prayer-man-kneeling-outside-sunlight-creativeswap.JPG?w=1200

SIKU YA NANE: ROHO MTAKATIFU NA UHAKIKA WA WOKOVU WAKO.

“Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia Neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, NA KUTIWA MUHURI NA ROHO YULE WA AHADI ALIYE MTAKATIFU.”
(Waefeso 1:13).
“ROHO MWENYEWE HUSHUHUDIA pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, na kama tu watoto basi tu warithi; Warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.”
(Warumi 8:16-17).
MAMBO YA KUJIFUNZA
1. Kila mtu aliyeokoka (kuzaliwa mara ya pili) ameokoka kwa njia au kwa msaada wa Roho Mtakatifu (Yohana 3:3,5).
2. Kila mtu aliyeokoka anaye mwalimu anayemfundisha ndani yake aitwaye Roho Mtakatifu (Yohana 14:26).
3. Kila mtu aliyeokoka amepigwa muhuri moyoni mwake wa Roho Mtakatifu wa kumtofautisha na wasio na Yesu (Waefeso 1:13).
4. Roho Mtakatifu ndani yako ndiye anayekuongoza na kukutia katika kweli yote (Yohana 16:13).
5. Roho Mtakatifu ndani yako ndiye anayekupa ndani yako mambo yakupasayo kufanya (Yohana 16:13-15).
6. Roho Mtakatifu ndiye anayekupa uhakika wa wokovu wako (Warumi 8:16-17).
MAOMBI
1. Muombe Roho Mtakatifu ndani yako akupe ujasiri na kujitambua kama mwana wa Mungu.
2. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kudumu kuyatenda mapenzi ya Mungu maishani mwako.
3. Muombe Roho Mtakatifu akukumbushe kila muda kuwa wewe si wa ulimwengu huu, ni mwana wa Mungu aliye hai.
Umebarikiwa,

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »