NJIA ZA MKATO ZA MAFANIKIO ZIPO KWENYE MAISHA, LAKINI ZIMEJAA VITA

“NJIA ZA MKATO ZA MAFANIKIO ZIPO KWENYE MAISHA, LAKINI ZIMEJAA VITA, NI WALE TU AMBAO TUKO TAYARI KUPAMBANA, KUFANYA VURUGU, KUSHINDANA, KUPIGANA, KUTOJIHURUMIA, KUJIHATARISHA NA KUTOJALI KELELE NA MANENO YA WALIOSHINDWA NDIO TUTATUMIA MUDA MCHACHE KUFANYA VITU AMBAVYO WATU WATATUITA FREEMASON NA MAJINA MENGINE MENGINE YASIYOVUTIA WALA KUPENDEZA! NA MIMI SIJALI LOLOTE, MIMI NI MTU WA VITA, NIITE JINA LOLOTE, NITAJE KWA KASHFA YOYOTE, LAKINI NITAKUJIBU KWA MATOKEO YASIYOHITAJI MAELEZO, YANAYOONEKANA WAZI KULIKO UMRI WANGU, MUDA NILIONAO KWENYE HUDUMA, UWEZO WANGU WA ELIMU YA DARASANI AU FEDHA…”
Askofu Dickson Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI

Kutoka 13:17
[17]Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, MUNGU HAKUWAONGOZA KWA NJIA YA NCHI YA WAFILISTI, IJAPOKUWA ILIKUWA NI YA KARIBU; maana Mungu alisema, WASIJE WAKAGHAIRI WATU HAWA HAPO WATAKAPOKUTANA NA VITA, na kurudi Misri

NIPO TAYARI KWA VITA DHIDI YA

 1. Shetani na majeshi yake, na matokeo yanajulikana nashinda mimi hata kabla ya pambano
  Yakobo 4:7-8, Warumi 16:20, Luka 10:19, Ufunuo 12:11
 2. Watu waovu wanaoletwa na adui kwenye njia ya hatma ili kutuzuia, na nitawakatilia mbali kwa upanga niliopewa na BWANA!
  Zaburi 118:10-12, Zaburi 64:2, 1Petro 3:12, Zaburi 27:2
 3. Tabia zangu binafsi zisizofaa na dhambi ambazo zinaweza kunizinga au kunizuia na kunichelewesha kwenda mbali mbingu ziliponikusudia!
  Waebrania 12:1,4, Warumi 6:13, Warumi 8:5-17
 4. Nyakati na mazingira magumu ambayo yanakatiza ndoto za wengine wengi waliokusudiwa mema na Mungu!
  Zaburi 23:4, Isaya 43:1-2, Waebrania 12:2-3
 5. Uvunjaji kanuni za mafanikio na kuishi kwa kanuni na nidhamu kama tabia!
  Mhubiri 1:9, Isaya 28:10, Wagalatia 6:16
 6. Kujifananisha na kujilinganisha na wenzangu wanaofanya ninachofanya vizuri au vibaya! Au wenzangu wenye umri wangu wanaofanya vizuri au vibaya!
  Yeremia 1:4-5, Isaya 49:1-6, Mathayo 25:14-15, 2Timotheo 2:20-21, 2Wakorintho 10:12

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »