THE POINT OF CHANGE

Point of Change
(C) @johngibbons -Unsplash

Sehemu ipi kwa mwanadamu ambayo ikihusishwa tu inaleta mabadiliko kwenye Maisha yake jumla ; mabadiliko kwenye tabia , ndoa, uchumi , kutoka dhambini
Kwa utafiki wangu ;
nilifikiri mchungaji akinyosha
mkono akasema ;

Fireeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee Fireeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Kwenye akili, kwenye nywele, kwenye Simu , kwenye nguo, kwenye ndoa yako
Na watu wakaanguka chini wote ; nilifikiri wakiinuka kwasababu ya fire tabia zao zitabadilika , lakini ndio wanaendelea vizuri
Nilifikiri Mtu wa Mungu akisema
Touch Touch Touch
Na watu wakaanguka ; nilifikiri watabadilika tabia, lakini hoo mambo yanabaki pale pale

KINACHOLETA MABADILIKO
kwenye Maisha ya mkristo aliyeokoka
ni maamuzi : maamuzi ya kulitii neno la Mungu bila shuruti ndicho kinacholeta mabadiliko
Unaweza kumuita mshirika ukamwambia simama pale , ukasema In the mighty Name of Jesus Christ touch , na akaanguka , na pepo wakatoka lakini kama hajaamua kubadilika ( nothing will happen )
Jaribu kufikiri

#Mwanzo 4:6-7
[6]BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
[7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Mwanadamu wa Kwanza hakushauriwa na baba yake, hakushauriwa na mchungaji , Alishauriwa na Mungu moja kwa moja ( Jaribu kufikiri ) , Ni Mungu ndiye aliyemshauri
Tuangalie Mungu anamwambia Kaini
Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
( Mungu anamshauri kaini anamwambia
Hiyo dhambi kuishinda kuko NDANI uwezo wako )
Mimi nilifikiri kaini ataogopa na kuifanyia kazi sauti ya Mungu kwa kutetemeka LAKINI jamaa aliendelea mbele na kufikia
Lengo lake la kuua ( just imagine )

HAYA TUONGEE NAWATAALAMU WA LEO
Ukikaa kanisani unasikia maonyo ya Roho Mtakatifu juu ya hiyo tabia uliyonayo ambayo haimpendezi Mungu ( unachukua hatua gani ? ) Ukibisha , chunguza Kwanza moyo wako
Utagundua ile hali ya Kaini iko sana sana, watu wengi wanamsikia Mungu lakini wengi bado wanaendelea na kufuata uovu ( Hii ni hatari sana – you kill your life )
NITARUDIA TENA ! KITU GANI KINAWEZA KUBADILISHA MAISHA YA MTU
Mungu toka amemuumba mwanadamu na alimuumba mkamilifu ( ana akili timamu anaweza kufanya maamuzi ), hakuwahi kuingilia maamuzi yake
Pia pamoja na Roho Mtakatifu kukaa ndani yako lakini bado unaweza kumzimisha ( Waefeso 4:30 ) na Pia mwisho wa siku unaweza kumzimisha
1 Thesalonike 5:19 )

Maana yake pia pamoja na Roho Mtakatifu kukaa ndani yako una uhuru wa kufanya maamuzi unayotaka ( Au kutii au Kutokutii )
Mabadiliko ya Maisha yako wapi ?
Mabadiliko ya Maisha yako kwenye MAAMUZI , siku umeamua ndio siku Maisha yako yanabadilika Jumla .
AMUA KUTENDA SAWASAWA NA
ANACHOSEMA MUNGU UTAONA MAISHA YAKO YAKIBADILIKA
God bless you
Pastor Ibrahim Amasi
ABC KAHAMA
LivingWord|2020
Make a Living

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »