TUJIFUNZE KWA MAMA KUKU!

Hivi karibuni nimesoma kitabu chenye jina ‘Prayer made practical’ kilichoandikwa na Fredrick Pelser. Miongoni mwa mengi niliyojifunza kupitia kwa mwandishi huyo ni kutafakari ukuu wa Mungu Muumbaji kwa kila ninachokiona au kukisikia, hata siku nikikutana na wewe nitamtukuza Mungu kwa jinsi alivyokuumba na vipaji alivyokujalia.

Katika banda langu ninakofugia kuku wa kienyeji sawa sawa na Ayubu 8:7, kuna tetea moja ambaye alikuwa ni mwoga, pia alikuwa anapenda sana kula! Nikiingia bandani na chakula, anakuwa wa kwanza kufika na ana spidi ya kula kuliko wenzake, ukimsogelea anakimbia na ukimshika ana makelele.

Sasa imefika wakati ametaga mayai na hatimaye kaanza kuatamia. Lengo la kuatamia ni kuyapa joto mayai yake kwa siku zilizoamriwa ili uumbaji uendelee ndani ya mayai na mwishowe atotoe vifaranga.

Tetea huyu mwoga na mpenda kula alipoanza kuatamia tabia zake zimebadilika, huyu aliyekuwa mwoga kwa sasa akiwa kwenye mayai yake ukimsogelea au hata kumshika habanduki, haogopi tena, hataki mzaha akiwa ameatamia akichuchumilia maono yake ya kupata watoto!

Hata chakula kiwe kizuri namna gani, ninapowapelekea bandani wenzake wanakimbilia, yeye hatoki kwenye mayai yake hadi wakati wake maalumu wa kula, hababaishwi na mtama, pumba na hata dagaa waliokuwa wakimpagawisha hapo mwanzo!

TUTAFAKARI PAMOJA:
-Kwa ubora jinsi Mungu alivyopenda mwenyewe kuumba, hatuwezi mujilinganisha na kuku kweli, lakini vipi unapokuwa umeweka lengo, unaweza kulisimamia mpaka mwisho bila kubabaishwa na vitu vingine?

-Kuku akiwa na lengo la kupata watoto alitafuta kiota akataga mayai, kisha akaanza mchakato wa kuvumilia kuyapa mayai joto kwa muda wa siku 21. Vipi wewe una lengo gani? Linahitaji nyenzo gani kulitimiza? Unadhani litakuwa limekamilika kwa muda gani? Katika kulitekeleza umeshaanza kuchukua hatua gani?

“Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.” (Mithali 29:18)

Kumbuka: Kushindwa kupanga, ni kupanga kushindwa!

“Ewe mvivu, mwendee chungu,
Zitafakari njia zake ukapate hekima.
Kwa maana yeye hana akida,
Wala msimamizi, wala mkuu,
Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;
Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.”
(Mithali 6:6-8)

Ni Muisraeli namba 3
Alex E. Bubelwa
0758298888
0782910000

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »