Ufahamu wa kupata Maarifa

Mbegu uipandayo kichwani

Katika Sayansi, Madaktari Wanajua Kuwa Kuna Magonjwa Ambayo YANAWEZA KUISHI NDANI YA MTU Bila Hata Mtu Kuwa Na Dalili Za Tatizo Au Hata Wazo Kuwa Ana Shida Hiyo Mpaka Pale Ugonjwa Unapochukua Udhibiti Na Utawala Kwenye Mwili, Ndipo Matokeo Ya Ugonjwa Yanatokea Nje Na Mtu Anajua Kuwa Ana Tatizo.
Mfano Mtu Anaweza Kuwa Na Kansa Kwa Miaka Kama 8 Au Zaidi Lakini Akiwa Hasikii Dalili, Wala Maumivu Au Mabadiliko Yoyote, Hadi Pale Ikishasambaa Na Kujieneza, Ndipo Matokeo Yanaonekana Nje!
Hivi Ndivyo Ilivyo “KWA MTU ANAYETUMIA MUDA WAKE KUJIJENGA KWA KWELI ZA NENO LA MUNGU; KISHA KUANZA KUTENDA NENO NA KULIISHI KWENYE MAISHA YAKE; UKIRI/ LUGHA YAKE, KUWAZA KWAKE, MTAZAMO WAKE, NA KUTENDA KWAKE” Itachukua Muda kidogo Kabla Ya MATOKEO Kuanza Kuonekana Nje, Lakini Kadri MUDA UNAVYOSOGEA NA ANAVYOZIDI KULIISHI, LAZIMA LITAANZA KUTOA MATOKEO “NJE” Kwenye Maisha yake Ya Kila Siku!
Ndivyo Ilivyo Hata Kwa JENGO KUBWA NA REFU; Kabla Halijaanza KUJENGWA NA KUONEKANA; Unaanzwa Kwanza KUCHIMBWA MSINGI MREFU NA MKUBWA KWENDA CHINI SANA; KUMWAGA ZEGE NZITO NA KUWEKA NONDO IMARA; Halafu Baada Ya Hapo JENGO LINAANZA KUNYANYUKA NA WATU WANAANZA KUONA “MWONEKANO WA NJE” WA JENGO; LINAENDELEA KUPANDA NA KUONGEZEKA NA KUPENDEZA NA KUSTAWI Lakini “SIRI IKO KWENYE MSINGI IMARA ULIOCHIMBWA KWENDA CHINI SANA NA KWA UMAKINI”
Hiki Ndicho Kitu Kinachonifanya Niwe Na Jeuri Ya Kufanikiwa Kwenye KILA ENEO LA MAISHA YANGU; HUDUMA, MAHUSIANO YANGU NA WATU WENGINE, KWENYE NDOA, UCHUMI, FEDHA, AFYA Nakadhalika… NIMETUMIA MUDA SANA “KWENYE MSINGI” Maana “JUMBA LA MAFANIKIO” Nitakaloporomosha Juu Ya msingi “NI KUBWA MNO”
Ukikutana na mimi nikiwa “Mtu mkuu sana” Usije Kufikiri Eti NIMEANZIA PALE ULIPONIJULIA, Hapana… “NIMEFANIKIWA MUDA MREFU TANGU NILIPOFANYA UAMUZI WA KUWEKEZA KWENYE SIRI ZA MAFANIKIO ZILIZOKO NDANI YA NENO LA MUNGU”
Mwanampotevu HAKUPOKELEWA NA KUFANYIWA SHEREHE NYUMBANI PALE ALIPOFIKA KWA BABA YAKE; “ALIFANIKIWA TANGU PALE ALIPOANYA MAAMUZI SAHIHI YA KURUDI KUOMBA MSAMAHA KWA BABA YAKE”
Mwanamke Aliyetokwa Na Damu kwa Miaka 12 Mfululizo, HAKUPONYWA ALIPOGUSA VAZI LA YESU; “ALIFANIKIWA TANGU ALIPOAMUA VEMA KWENDA KUGUSA VAZI LA YESU”
Mafanikio Yako Yamefungwa Ndani Ya Maamuzi Yako Sahihi Au Mabovu Unayochukua Linapokuja Swala La “UJENZI WA MSINGI WA KILE UKITAKACHO KWENYE MAISHA”
Sasa Wewe Uko Busy Na Kununua Nguo Za 50,000 ama Kiatu Cha 70,000 Lakini Huwezi Kununua Kitabu Cha Mtumishi Wa Mungu chenye Siri Na Kanuni Za Maisha Cha 5000 tu, ama Huwezi kununua CD AU DVD YA MAFUNDISHO YA Sh 5000 au 10,000 ya Mtumishi Fulani Wa Mungu, Wala Huwezi Kutumia Vizuri Mtandao Wako Wa Intanet Kwenda Sehemu Kama Youtube Na Kutazama VIDEO Za Mafundisho Za Watumishi Na Wahubiri Za Kukujenga Na Kukusaidia; Ukiingia Hapa Facebooka Uko Busy Kwenye Page Za UDAKU, MAPENZI, NGONO, PICHA NA VIDEO ZA UTUPU Na Bado Unataka Ufanikiwe; Huwezi Kufanikiwa UMEKOSEA KUJENGA MSINGI; UMEPANDA MBEGU ZA UHARIBIFU; LAZIMA UTAKWAMA…MAISHA LAZIMA YATAKUTOZA KODI!

Mwl D.C.K

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »