UNAJUAJE UNA KESHO KUBWA?
1. Unapoamua kwa dhati kuishi maisha matakatifu mbali na dhambi hasa DHAMBI ZA ZINAA NA UASHERATI
Watu wote wakuu wameshinda uchafu wa kingono, na kesho zao zikawa za utukufu!
Mwanzo 39:7-10
•Ayubu
Ayubu 31:1
•Mama wa Suleman alimjenga kwenye msingi huo, ingawa baada ya kuwa Mfalme aliuacha
Mithali 31:1-3
WAFUATAO KESHO ZAO ZILIHARIBIWA NA NGONO
•Reuben
Mwanzo 49:3-4
•Samson
Waamuzi 16:1
• Amnoni
2Samweli 13:1-39
KAMA UNA MPANGO WA KUWA MTU MKUU
•Usiendelee na dhambi za ngono, unaua ukuu wako
•Tafuta msaada ufunguliwe jumla na kushinda huu uovu
•Kama haujaingia kwenye dhambi hizi, jitunze kwa dhati mbali na hii dhambi, na itakusaidia mno kuiendea kesho yako ya ukuu kwa ujasiri
• Condom zinaweza kuzuia mimba, lakini haziwezi kuzuia utendaji wa nguvu za giza kupitia uhalali uliowapatia kwa kuzini
•Vizuia mimba na teknolojia ya kuzuia mimba havitoshi kukutia moyo uone zinaa ni kawaida, ni kitu cha kiroho, unauza kesho yako ya utukufu!
MWENYE MASIKIO NA ASIKIE,
KILA SIKIO LA KUFA NA LISIKIE DAWA,
Askofu Dickson Kabigumila
25.03.2024