“IPI NJIA RAHISI YA KUTOKOMEZA UMASIKINI AU KUKWAMUA WATU KWENYE UMASIKINI?”

“IPI NJIA RAHISI YA KUTOKOMEZA UMASIKINI AU KUKWAMUA WATU KWENYE UMASIKINI?”

JIBU LANGU

“Njia rahisi ya kukwamua watu kwenye UMASIKINI ni WEWE MWENYEWE KUTOKUWA MASIKINI kwanza”

ANAYEHOJI: KI VIPI? FAFANUA HAPO BISHOP

UFAFANUZI WANGU

1. Ukifanikiwa wewe kwanza kutoka kwenye umasikini, kwa hilo tu UMEPUNGUZA IDADI YA MASIKINI TAYARI, kuna masikini mmoja umefanikiwa kujitoa kwenye gereza na kupunguza msongamano! Kadri mtu mmoja anavyokazana yeye na kutoka, namba ya masikini inazidi kupungua!

2. Ukifanikiwa wewe kwanza kutoka kwenye umasikini, kwa hilo tu SAUTI NA HEKIMA YAKO itapokelewa kwa uzito na masikini kwa sababu MATOKEO HAYAJAWAHI KUPUUZWA na maandiko yanasema, HEKIMA YA MASIKINI HUDHARAULIWA NA MANENO YAKE HAYAPOKELEWI (Mhubiri 9:16).

3. Ukifanikiwa wewe kwanza kutoka kwenye umasikini, MAISHA YAKO YANAKUWA MFANO HAI NA KIOO NA HAMASA KWA MASIKINI WALIOBAKI KUWAPA IMANI KWAMBA INAWEZEKANA!

Ni rahisi kusikia mtu anasema, “Hata Bakhressa alianza akiuza kahawa Kariakoo na akatoka, na sisi tutatoka tu”

Mafanikio ya mwingine aliyetoka chini huku wengine wakimtazama, ni kichocheo cha wengine kuamka!

4. Ukifanikiwa wewe kwanza kutoka kwenye umasikini, inakupa urahisi wa KUONESHA HURUMA NA UPENDO WAKO KWA WENGINE KWA VITENDO, MAANA MASIKINI HAWEZI KUINUA WENGINE KWA VITENDO HUISHIA KUTAMANI BILA UWEZO WA KUCHUKUA HATUA KWA SABABU YA UKOSEFU WA RASILIMALI!

Tukazane sisi kwanza tutoke chini, ndipo tuwavute wengi waje kwetu juu tulipo!

5. Ukifanikiwa wewe kwanza kutoka kwenye umasikini, utaweza kutoa wengine wengi chini kwa urahisi kwa sababu utakuwa UMEJUA KANUNI ZIPI ZINAFANYA KAZI NA ZIPI HAZIFANYI KAZI KWENYE MAFANIKIO, NA UNAWEZA KUZISAMBAZA KWA WENGI KWA WAKATI MMOJA NA WAKAPATA NURU KULIKO UKIWA BADO MASIKINI!

Tukazane tu tujikwamue sisi kwanza, huu ni msaada mkubwa mno kwa wengine!

NIKAHITIMISHA HIVI

“Kufanikiwa kwa Lazaro kuwa tajiri ni kupunguza idadi ya akina Lazaro wanaogombea makombo chini ya meza ya tajiri”

Askofu Dickson Kabigumila

ABC GLOBAL DUNIANI

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »