MAOMBI NA USHAURI KWA WENYE “MAWAZO, MIPANGO, NDOTO NA MAONO

maombi
maombi

Nitakuwa Na Maombi Maalumu Kwa Ajili Ya Wale Wenye Mawazo, Mipango, Ndoto Na Maono Ya Kutimiza Mambo Fulani Ndani Ya Mwaka Huu 2014.
Ni Maombi Kwa Ajili Ya Wale Wenye WAZO LOLOTE AU MPANGO WOWOTE WA KIMAENDELEO Na Kwa Wale Ambao Wana NDOTO, MAONO Ambayo Wamekusudia Yatimie Mwaka Huu 2014.

MASHARTI NA VIGEZO KUZINGATIWA:
Mimi Sio MASHINE YA MAOMBI [Prayer Machine] Na Hivyo Sitachukua Maombi Yako Na Kuanza Kuyaombea Mfululizo BILA WEWE KUSHIRIKI.
Mimi Nitakuwa Tu PRAYER PARTNER WAKO [Mshirika Wako Kwenye Maombi]!

NAMNA YATAKAVYOFANYIKA:
1.Utatuma Kwangu Maombi Yako [Kwa Meseji Na Kwa Email]
2.Utanipigia Simu Kwa Ajili Ya Maongezi Mafupi Na Ushauri Na Kupeana Majukumu Ya Namna Ya Kuomba
3.Orodha Ya Maombi Utakayonitumia, Hakikisha Na Wewe Umebakiza Copy Au Umeyaandika Kwenye NOTEBOOK Yako Ili Yakiwa Yanajibiwa, Una-tick Na Unaelewa Ni Kipi Bado
4.Ukiamua Kunishirikisha Maombi Na Mahitaji Yako, UTALAZIMIKA KUKUBALI KUWA CHINI YANGU [Kimaelekezo Na Ushauri] Kuhusu Namna Ya Kuombea Hilo Lakini Pia Namna Ya KUTIMIZA HIYO NDOTO/ MAONO
5.Itakubidi Uwe Unawasiliana Nami Walau Kila Baada Ya Siku 2 Kupeana UPDATE [Kinachoendelea] Na Kupeana Hekima Ya Kuendelea Mbele… Maana Yake Nitahitaji Kuwa Na Mawasiliano Ya Karibu Na Wewe.

Kama Unaona Unaweza Kufanyia Kazi Haya, Karibu, Leta Maombi Yako… Kama Unaona Huwezi, Basi Uwe Na Amani Na Ubarikiwe!
Nimeweka Mwongozo Huo Hapo Juu Kwa Sababu Sipendi Kufanya Mambo Ya Kubahatisha, Nataka Kujionea MATOKEO YA MAOMBI WAZIWAZI Na Pia Kumsaidia MWENYE MAHITAJI Kukaa Kwenye Uwepo Wa Mungu!

Mwl D.C.K
E-mail
dicoka@rocketmail.com
Simu
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »