MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 9]

ROHO MTAKATIFU NA UPONYAJI.

MAANDIKO:

“Habari za Yesu Kristo wa Nazareti, jinsi Mungu alivyompaka mafuta kwa ROHO MTAKATIFU NA NGUVU, akazunguka huku na huko akitenda mema NA KUPONYA WOTE WALIOONEWA NA IBILISI, kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye.”
(Matendo 10:38).

“Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima, na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;…. NA MWINGINE KARAMA ZA KUPONYA KATIKA ROHO YULE MMOJA…”
(1Wakorintho 12:7-9).

“Lakini ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu; Yeye aliyemfufua Kristo Yesu, ATAIUHISHA (ATAPONYA NA KUIPA UZIMA) MIILI YENU ILIYO KATIKA HALI YA KUFA KWA ROHO WAKE AKAAYE NDANI YENU…”
(Warumi 8:11).

MAMBO YA KUJIFUNZA;

1. Uponyaji ni matokeo ya nguvu za Mungu katika Roho Mtakatifu kutiisha roho za udhaifu (Luka 13:10-17).

2. Yesu pamoja na Mitume waliweza kutembea katika upako wa kuponya kwa sababu ya ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE (Matendo 10:38).

3. Kuna karama tisa anazotoa na anazotumia Roho Mtakatifu kumdhihirisha Yesu katika ulimwengu huu, mojawapo ni KARAMA ZA UPONYAJI, ambapo ROHO MTAKATIFU anajifunua rasmi kwenye eneo la kuponya (1Wakorintho 12:6-12).

4. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako na juu yako unaamua kiwango cha nguvu za uponyaji utakazotembea nazo (Matendo 1:8).

5. Roho Mtakatifu ndiye anayeligeuza Neno la uponyaji kuwa roho na uzima kwa mtu anayetumiwa kuponya au anayetaka kupokea uzima (Yohana 6:63).

6. Neno la Mungu ni upanga pekee ambao Roho Mtakatifu anautumia kuleta matokeo maishani mwa mtu, likiwemo suala la uponyaji (Waefeso 6:16-17).

KWA VILE UMEZALIWA MARA YA PILI (UMEOKOKA) TAYARI UMEZALIWA KWA ROHO (Yohana 3:3-8), hivyo umekuwa mwana wa Mungu kwa nguvu za Roho wa Mungu mwenyewe ambazo ukizitumia kwa imani, UNAWEZA KUTUMIWA NA MUNGU KUPONYA KILA UGONJWA (Marko 16:17-20, Matendo 19:11-13) lakini pia wewe mwenyewe kupokea UPONYAJI WA UGONJWA WOWOTE MUDA WOWOTE UKIHITAJI, KIKUBWA TU UAMINI (Warumi 8:11)!

MAOMBI

1. Kama una shauku ya kutumiwa na Mungu katika eneo la uponyaji, muombe Roho Mtakatifu akutumie kudhihirisha nguvu ya uponyaji ya Kristo Yesu.

2. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kutembea katika ushirika naye ili iwe rahisi kutumiwa naye kufanya kazi zote alizofanya Yesu, ikiwemo uponyaji wa kila namna ya ugonjwa na udhaifu (Yohana 14:12)!

3. Kama ulikuwa na ugonjwa au udhaifu wowote, komaa na ushahidi wa Neno la Mungu ya kuwa ROHO MTAKATIFU ALIYEMO NDANI YAKO, ALIYEMFUFUA YESU TOKA KATIKA WAFU ana kazi ya kuponya mwili wako kila ukiwa na udhaifu wowote, hivyo komaa naye sawa na WARUMI 8:11, upokee uponyaji wa kila udhaifu na ugonjwa kwenye mwili wako!

NB: ANDAA SADAKA YAKO NZURI KWA AJILI YA MFUNGO HUU AMBAYO UTAITOA KESHO TAREHE 01/05/2019 SIKU YA KUHITIMISHA!

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »