MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -AUGUST [SIKU YA 3]

KANUNI YA MUDA/WAKATI (THE PRINCIPLE OF TIME).

Image result for checking a watch

Utangulizi.

Maisha ni muda, na muda ni maisha!
Hakuna maisha bila muda, maisha ya mtu au kitu yamefungwa kwenye muda!

Maisha ya mtu yamefungwa kati ya muda wa kuzaliwa na muda wa kufa (Mhubiri 3:2)!
Vitu pia vimefungwa kwenye muda au nyakati: Muda wa kuumbwa/ kutengenezwa na muda wa kuharibika/ kutoweka (manufacturing and expiring time)!

Kwa ujumla kila kitu duniani kinatawaliwa na kanuni ya muda.

Mimea inatawaliwa na kanuni ya muda pia; Muda wa kupanda na muda wa kuvuna (Mhubiri 3:2)!

Kila kusudi chini ya mbingu, alilonalo mwanadamu (alilobeba mwanadamu) limefungwa ndani ya muda (Mhubiri 3:1)!

Ukicheza na muda, umecheza na maisha yako.

Ukicheza na muda, umecheza na kusudi lako.

Ukicheza na kusudi lako, umecheza na maisha ya wengi waliokusudiwa kufaidika au kuponywa na kusudi ulilobeba!

Ndio maana maandiko yanatuhasa kuhusu matumizi sahihi ya muda, yakisema; TUUKOMBOE WAKATI/ TUUTUMIE MUDA KWA USAHIHI (Waefeso 5:16).

Yesu Kristo, Bwana wetu naye amesisitiza kuhusu muda akisema; YATUPASA KUFANYA KAZI MAADAM NI MCHANA, USIKU WAJA ASIPOWEZA MTU KUFANYA KAZI (Yohana 9:4).

Na akasisitiza kuwa MUDA TUWAPO DUNIANI, NI MUDA WA KUWA NURU YA ULIMWENGU (SULUHU NA MAJIBU KWA DUNIA YETU) NA SI VINGINEVYO: Yohana 9:5, Mathayo 5:13-16!

KWANINI NI MUHIMU KUZINGATIA KANUNI YA MUDA (KWANINI MUDA NI MUHIMU);

1. Hakuna maisha bila muda; maisha ya mtu au kitu yamefungwa ndani ya muda.
Ndio maana makaburini wanaandika jina la mtu na tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa na tarehe, mwezi na mwaka wa kufa.
Kwenye bidhaa yoyote rasmi, kuna muda wa kutengeneza na muda wa kuharibika (manufacturing and expering date)!
Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa (Mhubiri 3:2).

2. Kila kusudi limefungwa ndani ya muda, bila muda hakuna kusudi (Mhubiri 3:1).
Mipango, mikakati na malengo ya kutimiza chochote hapa duniani, yanatengenezwa ndani ya muda, yanatekelezwa ndani ya muda na yanatimizwa ndani ya muda.
Muda ni rasilimali ya lazima inayotawala kila kusudi chini ya jua!

3. Kila historia kubwa inatengenezwa ndani ya muda.
Hakuna historia isiyohitaji muda kutengenezwa.
Kila alama kubwa njema, isiyofutika na inayogusa vizazi vingi, inaachwa ndani ya muda wa uhai wa mtu au kusudi.

4. Utajiri au umasikini wa mtu, unaamuliwa na matumizi yake mazuri au mabaya ya kanuni ya muda.
Masikini ana masaa 24, kadhalika tajiri ana masaa 24 ya siku.
Wanachoamua kukifanya ndani ya muda ndicho kinachoamua yupi awe tajiri na yupi awe masikini.
KUWA MASIKINI AU TAJIRI SI BAHATI NI MATOKEO YA KUTUMIA VIZURI AU VIBAYA RASILIMALI YA MUDA.

5. Kila muujiza duniani umefungwa ndani ya muda.
Muujiza wa aliyepooza kwa miaka 38 pale katika kisima cha Bethsatha (Mathayo 5), muujiza wake ulikuwepo lakini ulifungwa ndani ya muda.
Mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka 12 mfululizo (Marko 5:25-34), muujiza wake ulikuwepo lakini ulifungwa ndani ya muda.
Baltimayo kipofu, aliyepiga kelele akisema YESU MWANA WA DAUDI UNIREHEMU, muujiza wake ulifungwa ndani ya muda.
Kila muujiza umefungwa ndani ya muda, unaweza kuchelewa lakini mhusika akiamini, hakika atapokea muujiza wake ndani ya muda sahihi uliokusudiwa!

6. Kila fursa maishani, imefungwa ndani ya muda; Ukichezea muda huo husika na usichukue maamuzi, hiyo fursa inapita na inabakia kujilaumu (Wimbo 5:4-6).

Kuna watu walipata fursa ya kununua viwanja, mashamba (ardhi) maeneo fulani, miaka fulani, na wakasita kuchukua hatua, matokeo yake wamekuja kuvinunua kwa bei hata mara kumi yake, au hawana tena uwezo wa kuvinunua tena, wanabaki kujilaumu!

Kuna watu walikuwa na fursa za kusoma na kujiendeleza kielimu, lakini hawakuchukua hatua walipokuwa na nafasi, matokeo yake wamekuja kusoma ukubwani au hawawezi tena kusoma, mlango umeshafungwa!

Unaweza kupata nafasi ya kurejerea jambo, lakini huwezi kurudisha muda nyuma.
MUNGU AMEKIFANYA KILA KITU CHEMA KWA WAKATI WAKE (Mhubiri 3:11).

7. Muda unabeba uponyaji ndani yake.
Maandiko yanasema; HUENDA KILIO HUJA KUKAA USIKU, LAKINI KICHEKO NA FURAHA HUJA ASUBUHI (Zaburi 30:5).
Ikiwa na maana kinachotibu nyakati mbaya maishani ni uwepo wa kurasa za muda zenye kubeba uponyaji wa nyakati mbaya maishani mwetu.
Wazungu wanasema, “TIME HEALS EVERYTHING!”

USISAHAU;

1. Pasipo muda, hakuna kusudi, pasipo kusudi hapana maisha.

2. Zuri au baya lolote duniani, huhitaji muda.

3. Muda hauombwi toka kwa Mungu au kusomewa chuoni, kila mtu ana rasilimali hii iitwayo muda mara ajapo duniani!

4. Matumizi mazuri au mabaya ya muda wako yataamua uzuri au ubaya wa maisha yako na vizazi vyako!

5. Matumizi sahihi au mabaya ya muda yataamua ukuu au uwastani au udogo wa maisha yako!
Nakushauri, UKOMBOE WAKATI (Waefeso 5:16).

6. Muda haurudi nyuma, unaweza kurejea kufanya ambayo hukufanya jana, lakini huwezi kurejeza umri na muda nyuma, tumia vizuri kila fursa ndani ya muda wake!
MUNGU ANAREJEZA MIAKA ILIYOLIWA, HAREJEZI UMRI (Yoeli 2:25).

7. Mbinguni tutahukumiwa kwa kazi tulizofanya/ kila kazi ya mtu itapimwa/ italetwa hukumuni (Mhubiri 12:14, 1Wakorintho 3:12-13).
Lakini KILA KAZI BORA AU MBOVU INAAMLIWA NA MATUMIZI YA MUDA (Yohana 9:4-5).

Kama una mpango wa kufanikiwa na kustawi hapa duniani na kuwa nyota mbinguni, usicheze na hii kanuni ya muda!

MAOMBI

ASUBUHI
1. Muombe Mungu akusaidie kutumia vizuri rasilimali ya muda aliyokupatia (Waefeso 5:14-17).

2. Muombe Mungu akusaidie kutumia vizuri kila fursa ndani ya muda wake ili usiwe na majuto utakapogeuka kuangalia nyuma ya miaka yako (Mhubiri 12:1-7).

MCHANA
3. Muombe Mungu akukutanishe na watu sahihi kwenye kila majira ya maisha yako, maana kila majira ya maisha yako yana watu aliokuandalia Mungu na walio na vitu vyako (1Samweli 10:3-4).

4. Muombe Mungu HEKIMA YAKE itakayokusaidia kutumia vizuri nyakati na majira maishani mwako (Yakobo 1:5-7, Zaburi 90:12).

JIONI

1. Muombe Mungu akurudishie KILA ULICHOPOTEZA NDANI YA MUDA FULANI WA MAISHA YAKO (Yoeli 2:25-27).

2. Muombe Mungu akusaidie KUCHUKUA HATUA SAHIHI NDANI YA MUDA SAHIHI (TO TAKE RIGHT STEPS IN RIGHT TIME) zitakazopelekea KUBADILISHWA JUMLA KWA MAISHA YAKO (Luka 15:17-24)!

MUHIMU

Usiache kuniombea mimi Mchungaji Dickson, familia yangu, kanisa la ABC, tuweze kutembea vizuri na Mungu katika muda aliotupa wa kuwa duniani!

Wewe ni mtu mkuu,
Uliyebarikiwa mno,
Umebeba majibu ya dunia yako,
Amua kuishi kuwa baraka kwa ulimwengu wako!

Tukutane kesho siku ya NNE!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji mwanzilishi,
ABC GLOBAL.

YOUTUBE Tafuta:

CHURCH STATION
NA

PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA

NIFUATE (FOLLOW) INSTAGRAM:
@mwalimukabigumila

Usiache kutembelea website yangu kujifunza zaidi:
www.yesunibwana.co.tz

NB: ANDAA SADAKA YAKO NZURI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU MWISHO WA MFUNGO KWA KADRI MUNGU ANAVYOKUPA KUPENDA!

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »