Unapolitumia NENO LA MUNGU Kama “SILAHA ILIYO NJE YAKO” Ni Sawa Itafanya Kazi Lakini “SI KWA KIWANGO NA UBORA UNAOTAKIWA” Na Hakika Hautapata Kiwango Cha Ubora Ambao Mbingu Zimekusudia Upate Kutoka Kwenye NENO.
Biblia Inasema, “UMEZALIWA MARA YA PILI KWA MBEGU ISIYOHARIBIKA, IDUMUYO MILELE, AMBAYO NI NENO LA MUNGU” (1Petro 1:23).
Kwa Lugha Nyepesi; Mara Tu Baada Ya Kuokoka, “WEWE UNAKUWA NA DNA [VINASABA] VYA NENO” Maana “NENO LA MSALABA” Ndilo “LILILOKUNUNUA PALE MSALABANI” Maana “NENO LILICHUKUA MWILI” Likaja Duniani Na “KUKUFIA MSALABANI” Na Ndilo Unalosoma Kwenye BIBLIA YAKO; Ukilitamka Na Kulitumia NENO LA MUNGU Kwa UHAKIKA NA IMANI “KAMA LAKO MWENYEWE” Badala Ya Kuliona Kama “ANDIKO KWENYE KITABU” Hakika Utashangazwa Na Ubora Na Matokeo Makubwa Yatakayoanza Kuzaliwa Maishani Mwako Kutokana Na NENO Maishani Mwako… NI NENO LA MUNGU NDIYO, LAKINI NI LAKO PIA MAANA WEWE NI MRITHI ULIYERITHI YA MUNGU [LIKIWEMO NENO LAKE] PAMOJA NA KRISTO YESU (Warumi 8:16-17).
Kwangu Binafsi Nikilitamka NENO, Natamka Kwa Uhakika, Nguvu, Mamlaka Na Pasipo Shaka Halafu Nasubiri Matokeo MAKUBWA Kama Ambayo Yangetokea Kama Lingetamkwa Na Mungu Mwenyewe!
“…KAMA YEYE ALIVYO, NDIVYO MIMI NILIVYO ULIMWENGUNI HUMU” (1Yohana 4:17).
MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 10]
KUISHI NJE YA UKANDA WA IBILISI (LIVING BEYOND DEVILS REACH) Ninasikia kuhusu maombi ya vita. Ni maombi maarufu ya kupigana na Ibilisi na majeshi yake.