“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na maono tofauti kabisa na ya familia mbili walikotokea… Wanapaswa kujua kilichowaunganisha na kukubali kuacha na kusahau kusudi na maono ya familia walizotokea ili kutimiza kusudi na maono yao… Watu wa familia hizi mbili walikotokea wanakuwa ni wageni waalikwa na wanaopaswa kukubali ukweli kuwa hawa wanandoa wapya walikuwa kwao lakini si wao tena… Tukielewa mipaka hii, tutapunguza matatizo ya ndoa kuvunjika kwa sababu ya wazazi na ndugu wa familia mbili tulikotokea… Mwanaume analazimika kuwaacha ndugu na wazazi wake na kuambatana na mkewe… Vivyo hivyo kwa mke (Mwanzo 2:24, Zaburi 45:10-11)“
Mafundisho
UKITAKA KUJUA ULIPO/ UNAPOABUDU KUNA KWELI YA MUNGU AU NI NJIA PANA IELEKEAYO UPOTEVUNI, ANGALIA YAFUATAYO;
1. Je msisitizo mkubwa mahali hapo ni INJILI YA KUGEUZA ROHO ZA WATU TOKA DHAMBINI AU NI KITUO CHA MIRADI, MIPANGO NA HARAMBEE ZA