“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa, ukubali Yesu akufungue, hiyo roho chafu ikuachie. Sasa ukioa kwa ajili ya kukimbia tamaa, je akiwa katika siku za hatari? Je akisafiri kikazi wiki mbili au mwezi? Vipi akiwa mjamzito na ana bed rest? Je akienda masomoni kwa miaka kadhaa? Haya ndiyo yanapelekea watu kuchepuka, kutembea na mashemeji, kutembea na mahouse girl. DAWA YA TAMAA SI KUOA, DAWA YA TAMAA NI KUFUNGULIWA KUTOKA HICHO KIFUNGO. Sasa puuza hii tutaonana mbele ya safari”
HEKIMA ZA NDOA 4
“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA