Mwamini Mungu Hata Kama Hatafanya Hilo utakaloo

shedrack
Shedraka, Meshaki na Abednego walijua siri hii ya ajabu. Walimjua Mungu wao. Walijua kuwa Mungu wao ni hai siku zote. Walijua anafanya kazi muda wote. Walijua yote yanawezekana kwake. Walijua yasiyowezekana kwao kama wanadamu, kwa Mungu wao, Jehova yanawezekana…WALIMWAMINI.
Hata ilipotokea JARIBU KUBWA KWAO LILILOGHARIMU MAISHA YAO…Bado walikuwa na Ujasiri wa kumwambia Mfalme Nebukadreza, “Mungu wetu tunayemwabudu aweza kutuokoa, lakini hata asipotuokoa na ijulikane ya kuwa hatukuisujudia sanamu yako” (Danieli sura ya 3).
Walikuwa na kiwango cha juu cha uelewa, walijua kuwa Mungu kutojibu Ombi lako sawa na ulivyomwomba haibadilishi Yeye kuendelea kuwa Mungu…Mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege amewahi kusema, “MUNGU ANABAKI KUWA MUNGU HATA KAMA HAJAJIBU OMBI LAKO KAMA ULIVYOMWOMBA”
Mungu asipofanya kile ulichomwomba, hasa pale unapokuwa umekiomba sawa na mapenzi yake [sawa na Neno lake] anakuwa na sababu…Pengine ameona kuna shida itatokea endapo ukipata kitu hicho na pengine utapoteza uhusiano wako na Yeye. Na kumbuka uhusiano wako na Mungu ni wa muhimu sana kuliko chochote mbele za Mungu…Pengine anataka kukupa kitu bora zaidi kuliko hicho ukitakacho sasa…Pengine anakuandaa kwa hatua fulani bora katika maisha yako..!
JIZOEZE KUMWAMINI MUNGU KATIKA HALI ZOTE, NJEMA NA MBAYA, NGUMU NA NYEPESI, KWENYE SHIDA NA RAHA…Haya ndiyo mapenzi yake kwako!

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »