Salamu nyingine kutoka Mwanza

Upako Unaweza Kukaa Kwenye Kitu Chochote Chenye Umbo Linaloeleweka [Physical Structure]… Unaweza Kukaa:
-Kwenye MIFUPA YA NABII ALIYEKUFA ELISHA Kiasi Cha Kuweza Kufufua Maiti
-Kwenye KIVULI CHA PETRO Hata Kuweza Kuponya Wale Waliojipanga Mitaani Wakimsubiri Enzi Za Matendo Ya Mitume
-Ulikaa Kwenye LESO NA NGUO Zilizotoka Kwa Paulo Na Kuponya Na Hata Kutoa Pepo
-Ulikaa Kwenye KIJITI KILICHOGUSWA NA NABII ELISHA Kilipotupwa Kwenye Maji Kikasababisha SHOKA Lililozama Likaelea
UPAKO SI ISHU SANA; UNAWEZA KUKAA JUU YA YEYOTE “MWENYE KIU NA NJAA YA NDANI YA KUTUMIWA NA MUNGU” Na “ALIYELIPIA GHARAMA KUKAA MBELE ZA MUNGU MPAKA AUPOKEE”
Tatizo Linakuja WATUMISHI WENGI “WANAANZA VIZURI” Wakiwa WAOMBAJI, WAFUNGAJI, WASOMAJI WA NENO, WAFUNDISHAJI NENO LA KWELI Lakini “WAKISHAPATA UPAKO” Wanaachana Na Mungu [CHANZO] Na Kuanza “KUUTUMIA UPAKO” Kwa MASLAHI YAO NA TAMAA ZAO..!
Na Inachukua Muda Sana UPAKO ALIOUPATA MTU Kupotea Au Kuacha Kufanya Kazi kwa Vile “KARAMA NA WITO WA MUNGU HAVINA MAJUTO” Hivyo MIUJIZA INAENDELEA, MAAJABU YANATOKEA Ingawa MTUMISHI HUSIKA [BINAFSI] Tayari AMEPOTEZA UHUSIANO NA MUNGU, Na ANAELEKEA JEHANAMU!!
Kama Mungu Alitumia MIFUPA ILIYOOZA YA NABII ELISHA KUFUFUA, Anaweza Kumtumia Yeyote Au Chochote… Usimpime MTUMISHI KWA IDADI YA MIUJIZA AU PEPO ANAOTOA, Angalia Na MAISHA YAKE :
1.Je Ni Mtakatifu, Na Anahubiri Na Kusisitiza Utakatifu??
2.Anaishije Na Watu Wanaomzunguka [Familia Yake, Majirani, Nk]? Je Ni Kielelezo Kwa Watu Katika Mfumo Mzima Wa Maisha Yake??
3.Lugha Yake Ni Ipi Na Ya Aina Gani?
4.Anatafuta Roho Za Watu Au Umaarufu Na Mali??
5.Ana Kiu Na Njaa Ya Kuona Watu Wanaokolewa Au Yuko Busy Kutangaza Kanisa Lake Na Dhehebu Lake??
6.Mahusiano Yake Na Watumishi Wengine Wa Mungu Yakoje?? Anawapenda Au Anashindana Nao??
7.Analegeza Ukweli kwamba Yesu Kristo Ni Njia Pekee Ya Uzima Wa Milele Au Anasimamia Hilo??
8.Anataka Tu Kanisa Lijae Au Anahakikisha Anawaandaa Watu [Kanisa] Lisilo Na Mawaa Tayari Kwa Umilele Wao??
9.Anasimamia Maslahi Ya Ufalme Wa Mungu Au Analinda Na Kutafuta Umaarufu Wa Jina Lake??

Ni Salamu Zangu,
Kutoka Mwanza,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »